March 04, 2011

Familia halisi/ ya kwanza

Neno familia sio geni kwenye masikio ya walio wengi, kwa tafasiri rahisi, "linamaanisha kizazi kimoja ambacho kimechipuka kutoka katika shina mmoja", kihistoria neno familia litakuwa na maana pana zaidi na pengine mwonekano mwingine, ila kwa hapa pengine linaweza maanisha  "..kichipuo kinachoanza na baba na mama ama wapendwa wawili wanapoamua kuanza maisha yao ya unyumba". Wakati mwingine huwa tunajiuliza kwa nini mtu anaamua kumtafuta msichana ama msichana anaamua kumtafuta mvulana wa kuishi naye ambao hatimaye wanaanzisha familia yao? Kwa kidini huwa twasema kuwa Mola/Mungu kajibu maombi hasa baada ya mvulana ama msichana kwa wakati wake kumuomba Mungu amjalia mchumba wa kufanana naye ambao kwao wanaanzisha FAMILIA. Kwa maneno matakatifu tunasoma kuwa binti ataondoka kwao na kumfuata mwanaume ama kijana ambao kwao wataanzisha maisha ya familia.... Je wewe maisha yako ya familia yalianzia wapi? Swali hili la tafakari, lakini je ni kweli kuwa yaliyosemwa katika maandiko matakatifu yanapimika ama vipi? Kwa waafrika walio wengi mwanaume ndiye anayechumbia na si binti kumchumbia mwanaume..." Je suala la mfumo dume labda lilianzia katika maandiko matakatifu? ingawa hii kwa wanaujinsia wanaweza kuwa na tafasiri nyingine ambayo itajadiliwa katika makala ijayo. India wanawake ndio wanaokwenda kucchumbia mwanaume lakini suala la mfumo dume lipo halipo? jibu....

Je kwako familia halisi nini? familia halisi ama familia ya kwanza ilianza tangu mungu alipoumba Adam na Hawa na kuwakabidhi bustan ya Eden waitunze kabla ya nyoka hajamdanganya Hawa ili walitumie ama kula tunda la kati kati ya bustani....

Itaendelee..

No comments: