June 14, 2013

Mahusiano na Mapenzi

Habari wanafamilia, leo naona nianze kusema nanyi kuhusu sula la Mahusiano na Mapenzi.

Ni kweli ukiwa na mpezi wako lazima mfanye ngono? ama ukimkatalia anasema nakupenda ila nitatafuta msichana mwingine ambaye ataniridhisha na kutimiza haja yangu ya kingono!

Maswaibu haya na mengine mengi yamekuwa ni mambo ambayo yanawaumiza hasa wasichana wengi... kuliko wavulana... eti msichana akipata mimba nani anaumia kati yake Msichana na Mvulana?

Bila shaka ni msichana, anaanza kuwaza sasa jamaa asiponioa nitakuwa mgeni wa nani? je wazazi wangu nitawaambia nini? na wakiniuliza mimba ya nani nitasemaje? kibaya zaidi urafiki wenu hamjauonesha kwa wazazi...

Kwa wasichana wanaumia sana na wavulana inakuwa ni kuonesha kwa masela kuwa yeye ni kidume/dume la mbegu... huu ni utoto wakati mwingine...kwani ukianzisha urafiki/mahusiano na msichana lazima muishie kufanya ngono? yapo mengi ambayo mnaweza kufanya mkiwa wote na kuridhishana kimahaba.....na kila mtu akalizika.... ila kwa hivi sasa suala hili linaoenekana ni gumu kwa vijana....

Vijana wengi wanakuwa na urafiki wa ushabiki na ukisha lala nae ama kufanya nae ngono ujue anaweza kukimbia!

Ushauri ni kuwa jitahidi kusubiri na kujiepusha na vitendo vya ngono ili mtimize ndoto zako..wakati mwingine unaweza kuwa na wasiwasi kuwa anaweza kunikimbia eti sijampa kile anataka! hasha, kama ipo ipo tu! Wahenga walisema kuwa "Wasiwasi nayo nia akili"

Ama mkishindwa kabisa tumia kondomu, ila mazungumzo yatawale hisia zenu

By Mutasingwa

No comments: