June 21, 2013

Kwa nini usiolewe eti....

Usiolewe eti kwa kuwa rafiki zako wengi wameolewa

Usiolewe kwa kuwa eti umemaliza chuo na una kazi nzuri

Usiolewe eti kwa kuwa mama na baba wanataka mjukuu

Usiolewe eti kwa kuwa marafiki zako wanataka kula Ubwabwa wa shughuli yako

Usiolewe kwa kuwa una gari zuri na maisha umeanza kuyapatia!

Usiolewe kwa kuwa wachungaji kanisani wanakuulizia eti na wewe unaoelewa lini?

Usiolewe kwa kuwa rafiki wa kiume wa kwanza kapita bila bila wapili, watatu, wanne wote kimya.... unaona kama umesahaulika...!

Usiolewe kwa kuwa umebeba mimba....ya huyo boyfriend wako ambaye uliyenaye....ilihali unaona kuwa hamtafika mbali....

Olewa baada ya Mungu kujibu maombi yako na kukupatia Mume mwema, utamjuaje ni mume mwema....?

Itaendelea toleo lingine....

By Mutasingwa 

No comments: