June 07, 2013

UNYANYASAJI WA KIJINSIA

Unyanyasaji wa kijinsia, unachangia kwa kiasi kikubwa vifo kwa akina mama na watoto, maeneo ambayo vitendo hivi vimekithiri kwa Tanzania ni Mkoa wa Mara, wakati fulani nilikutana na Binti jina kapuni, alipigwa na mzazi wake kiasi kwamba ukiaangalia picha hizi utastaajabu kama kweli aliyetenda haya ni mzazi wa kumzaa.... sababu ya haya yote ni binti kuchelewa kurudi nyumbani akitokea matembezi ya sikukuu....ndipo mzazi alipoamua kumchapa fimbo akiwa amelala kifudifudi sehemu za mgongoni kwa zaidi ya saa mmoja.... hebu jiulize unyama na ukatili huu ulikuwa ni kiasi gani

 Ukiangalia picha hizi sio nzuri, ila kwa idhini ya mtedwa alisema kuwa zitumike ili jamii ione jinsi wazazi wanavyoweza kuwa zaidi ya binadamu wa kawaida....

Suala ambalo lilishangaza wakati wa mahojiano, mtoto alionesha kuridhika na kuonesha kuwa anamuachia Mungu haya yote..... Mie najiuliza ukatili huu mpaka lini?....

Hebu jamii na vijanakwa ujumla tufunguke na kusema hapana kwa ukatili wa aina hii

Labda tukumbushane haki zetu ambazo ni nadondoa kwa kiasi.....
1. Haki ya kuishi
2. Haki ya kulindwa
3.Haki ya kuheshimiwa na kutunziwa siri
4.Haki ya kupatiwa elimu
5. Haki ya kupatiwa huduma bora za afya
6. Haki ya kutoa maoni na kusikilizwa
7. Haki kucheza.....

Hapa kwa ufupi mzazi alikiuka haki ya kulindwa, na pengine kutishia pia haki ya Uhai kwa maana ya haki ya Kuishi. huyu alitakiwa kufikishwa mikononi mwa Dola na sheria kuchukua mkondo wake.....


By Mutasingwa

No comments: