Tangu ulipogunduliwa Ugonjwa wa UKIMWI, miaka ya 80s serikali ilianza jitihada za kupunguza maambukizi, ilianza suala la kuhamasisha vijana kubadili tabia, suala hili limeonekana kuwa gumu, kiasi kwamba tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa vijana wanaanza vitendo vya ngono wakiwa na miaka 10 hivi, kiasi kwamba kushindwa kujua hasa nini chanzo, harakati mbalimbali zimeendelea kwa wadau wote NGO, mashirika ya kidini na mengine kemkem,na wadau wa maendeleo bado jitihada zinaendelea maana vijana wanaonesha kutosikia la mkuu wala la Mhazini.... jambo hilo ndio linalo nisukuma kuona leo nijadilia kwa nini kondom kwa vijana.
Zipo sababu kadhaa ambazo zinaashiria vijana kuanza vitendo vya ngono mapema
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na TACAIDS na NIMR wa 2011, mikoa ya Dodoma, na Mbeya umeonesha kuwa vitendo vya ngono vinaanza mapema kwa vijana wa kike na kiume, ripoti ya viashiria vya UKIMWI nchini kwa mwaka 2011/12 ya mwezi februari mwaka huu, imeonesha kuwa maambukizi ya UKIMWI kwa vijana kati ya miaka 15-19 na matokeo yake kuanza kujionesha miaka ya 23-24, aidha, maambukizi ya watoto wa kike ni asilimia 6.6 na kiume ni asilimia 2.8, kwa maana hiyo wasichana walau ni mara mbili ya watoto wa kiume.... hii ni hatari kwa ustawi wa jamii na upotevu wa nguvu kazi ya baadaye. Bado kondom haineshi kuimalika kwa watoto wa wa jinsi zote si kike au kiume!
Pili, masuala ya afya ya uzazi na ujinsia imeonekana ni miiko kuzungumwa katika jamii yetu, wakati tafiti zinaonesha kuwa endapo wazazi/walezi watazungumza masuala haya kwa uwazi, kunauwezekano wa kupunguza maambukizi ya UKIMWI kwa asilimia 0.9, je kipi bora?
Tatu suala la matumizi ya kondom, imeoneka ni msamiati kwa vijana.... hii inatokana na dhana potofu miongoni mwa vijana...eti kondom haina radha! eti ina baridi! eti ina vitundu vidogovidogo! eti inaweza kuzama wakati wa kujamiana.... je kipi bora? kuacha kabisa kutumia kondom kwa sababu ambazo hazipo kisayansi.... ama kutumia kujiepusha na madhara makubwa ya maambukizi ya VVU? hebu jitafakari na kuchukua hatua mapema kijana..
Aidha, muarobaini wa yote hayo ni kuanza elimu ya makuzi na malezi kwa watoto wakingali wadogo..kuanzia walau miaka 5 na kuendelea.... nini kifundishwe? itategemea kulingana na uelewa wa watoto... siku hizi utandawazi watoto wanaelewa sana sio kama enzi za MWAAALIM!
Wazazi na walezi wawalinde watoto na hatari ya kujiingiza katika ngono zembe na kuachana na Tamaa zisizo na msingi...jukumu la kuwalea watoto wako ni lako sio la mwingine...mkunje samaki akingali mbichi sio usubiri akauke itakuwa hatari...
ZINGATIA
A-cha kabisa ngono
B-akia na mwenzi mmoja
C-ondom ni muhimu ikibidi
By Mutasingwa
No comments:
Post a Comment