August 31, 2010

NGUVU ZA KIUME NI TATIZO KUBWA KIASI HIKI??

Kwa takriban miongo mingi kumekuwa na harakati za waganga wa kienyeji kujihusisha na uuzaji wa dawa za kuongeza nguvu za kiume, kurefusha size ya UUME, kuongeza mvuto wa mapenzi na nyingine nyingi, suala hili limekuwa likisheeni pia katika magazeti kwa njia ya matangazo, jaribu kusoma magazeti pendwa utakuta matangazo yasiyopungua kumi au kumi na tano tofauti, lakini pia katika mitaa mbali mbali ya jiji la DSM, utakutana na matambala yanayoashiria kuwepo mganga ambaye anatibu matatizo haya! Sasa najiuliza je suala hili ni kibwa kiasi hiki wa baadhi ya wanaume? Je dawa hizi zinazotumika zinasaidia ama kuondoa tatizo hili kwa asilimia ngapi? Pengine mie nalitazama kama suala la kujiongezea kipata linalotokana na ubunifu wa baadhi ya waganga wa kienyeji! Hivi ni kweli kuwa watu wengi hasa wanaume wanashindwa kuwafikisha  wapenzi wao KILELENI kwa sababu tu wanamaumbile madogo? au kukosa nguvu za kiume? hivyo kuhitaji dawa na matibabu hayo? Wengine wanaaamini kuwa ukinya mchuzi wa PWEZA AU MTABIRI basi  utaweza kwenda zaidi ya kawaida na kumfikisha mwenzi wako kileleni!!! ya kweli hayo?

Tujadiline kidogo na kupeana uzoefu.... ili tuwasaidie wanafamilia waumini wa dawa hizi...

No comments: