Kuna taarifa imetufikia asubuhi ya leo kuwa hapa Dar maeneo ya Sinza Lion kuna msiba wa baba mmoja ambae amefariki jana baada ya kuugua kwa wiki moja.
Sasa maajabu yaliyojitokeza ni kwamba watu wakilia nyumba inachuruzika damu kutoka juu kwenye paa na ukutani kwenye matofali.Ikabidi waite wachungaji kwa ajili ya kuomba na kukemea hiyo hali kwa hiyo wachungaji wakafika pale na kuanza kukemea na damu kuacha kuchuruzika.Ila wakiacha tu kusali na wafiwa kuendelea kulia damu inachuruzika.
Gea Habib amekwenda pale kutoa pole kwa wafiwa na kupata hiyo habari lakini imeshindikana kupata picha kabisa maana kuna ulinzi hawataki waandishi wa habari asije kupigwa bure.Inasasemekana damu ilikuwa inatoka sebuleni na nje kibarazani ukiwa unaingia ndani.Ila ananiambia kwa sasa damu imeacha kutoka ila ipo iliyoganda ukutani wafiwa wanajaribu kufuta.Jamani ni maajabu haya wala si uongo sikiliza kesho katika hekaheka za leo ndani ya leo tena.
Kutoka dinamarios.blogspot.com
No comments:
Post a Comment