April 21, 2010

VISA NA MIKASA YA WAISICHANA WA KAZI KUWENI MAKINI......

Salaaa, ndugu wanafamilia. Nimefanya utafiti kidogo na kugundua kwa sasa kuna watu wanaokwenda vijijini hasa mikoa ya Iringa, Mbeya, Morogoro, Tabora, Kagera, Singida na kwingineko kuwachukua wasichana, ambao mwisho wa siku wanafanyisha kazi za ndani yaani kwa ufupi madalali.




Hebu soma visa hivi:-



Kisa cha Kwanza:-Msichana wa kazi kukamatwa akiwa uchi chumbani kwa mabosi wake.

Siku mmoja mwanzoni mwa mwezi wa pili 2010, msichana wa kazi alikutwa anawanga katika chumba cha mabosi wake, alipokutwa na mtoto wa bosi, akiwa uchi wa mnyama alidai kuwa yeye alitumwa na bibi yake, popote atakapo kwenda kufanya kazi basi apate damu ya mtoto wa bosi yoyote yule, motto wa bosi alipiga kelele na kuwaita majirani ili kupata msaada, ndipo majirani walipomchukua na kumpeleka kituo kidodo cha polisi StakiShari Ukonga, baada ya kugundua kuwa nyumba hiyo ilikuwa inalindwa na damu ya YESU, anasema kila wachawi walipokuwa wakija wanashindwa kuingia ndani wakidai kuwa kuna moto utawauguza, basi baada ya wazazi wa motto kufika wakapata taarifa ndipo walipochukua jukumu la kumfukuza msichana bila hata ya kumpa senti yoyote.



Kisa cha Pili:- Msichana wa kazi amua mtoto wa mwenye nyumba wa miezi nane …..

Mama mmoja alitumiwa msichana wa kazi kutoka Songea vijijini, na aliyemtuma yule msichana inadaiwa alikuwa rafiki wa mke mwenza wa yule dada aliyeletewa msichana, baada ya kufika Dsm (Ukonga Mombasa) binti yule alianza kazi yake ya kumlea mtoto, baada ya siku mbili akaanza kuchoma ubani kila asubuhi wakati wenyeji wanapokwenda makazini, mara ananunua udi na kujifukizia, mara anaamka asubuhi amechanjwa na matukio kadha wa kadha, siku mmoja mama mtoto aliamka asubuhi akamkuta anachoma ubani, alipomuona, akazima harakaharaka ili asigundulike, alipoulizwa akasema hafanyi kitu, baada ya muda uji ulipoiva akaanza kumnywesha mtoto, inadaiwa mtoto alipewa kiasi vijiko viwili/vitatu, ghafla, mtoto akaanza kubadilika na kutokwa mabovu mdomoni, puani na kuhema taratibu, mama yake alipofika akamkuta mtoto akiwa katika hali mbaya, ndipo alipoulizwa umemfanyaje mtoto? akasema "kuwa amempa uji vijiko viwili ghafla, akaona mtoto ameanza kubadilika". Mama mzazi wa mtoto alichukua teksi haraka na kumkimbiza hospitali ya AMANA iliyopo Ilala, alipofika mtoto amelegea, alipoulizwa na nesi, akasema mtoto kabadilika alipoanza kupewa uji wala hakuwa na dalili yoyote ya kuumwa. Ndipo, alipoingizwa chumba cha wagonjwa mahututi ili kufanyiwa uchunguzi, manesi walihangaika kujaribu kumuingizia mirija mtoto puani ili walau kubaini tatizo, kila wakiingiza mirija vinatoka vitu vyeusi mithiri ya sumu. Tukio hilo lilianza saa 2 asubuhi, basi, mtoto akaendelea kupewa huduma ya dhalura, ilipofika muda wa mchana akanza kupata nafuu ila akiwa hana nguvu, ilipotimu muda wa saa tatu usiku mtoto akakata roho. Mtoto huyo alikuwa na umri wa miezi nane tu..., baada ya kufika nyumbani siku hiyo hiyo, msichana wa kazi akaulizwa imekuwaje ndipo alipoanza kuelezea kuwa yeye kule Songea alikuwa na bibi yake ambaye alimuingiza katika kazi ya uchawi, hivyo alipoondoka aliambiwa akatafute wafuasi, hasa watoto, alipotamka hayo nyumba nzima ikazizima kwa vilio, ghafla wanapokea taarifa kuwa mtoto amefariki dunia, Msichana huyo, aliendelea kusema kuwa, hata siku alipoamka amechanjwa, bibi huyo aliyemtuma, wachawi walimjia kutaka kujua kulikoni mbona hatekelezi maagizo aliyopewa kabla ya kuja kuanza kazi DSM? Binti huyo, akaendelea kusema kuwa ndipo waliponichanja na kusema kuwa wakifika kabla sijatekeleza wataniua,..., baada ya maelezo hayo ndugu na majirani wa karibu wa familia hiyo walipotoa ushauri ya kuwa atafutwe mchungaji ali aendeshe maombi, katika familia hiyo wao ni wakristu safi, ila shetani kama kawa akatia nanga, Baada ya kufika mchungaji akanza maombi ndipo alipotamka mengi zaidi, msichana huyo akapandisha mashetani na kusema “kuwa yeye ametumwa kuimaliza familia hiyo, amekabidhiwa dawa nyingi ambazo ameziweka katika maeneo mbali mbali ya nyumba na amepewa kisu cha kuchinja wanafamilia kila baada ya mwaka fulani...akaendelea kusema kuwa vitu alivyopewa ni vingi hawezi kuviondoa vyote humo ndani mpaka apate msaidizi atakaye kuja usiku hivyo apewe muda ili akija wavitoe, alipoulizwa kuhusu kumua mtoto alidai kuwa mtoto bado hawajamchukua yupo AMANA ila kesho wanatarajia kumvunja vunja na kumpeleka Songea..... Kesho yake wakati ndugu na jamaa wanaanda taratibu za mazishi, alipoulizwa akasema kuwa mtoto wameisha mchukua, na ametishiwa hata yeye atauawa kwa kuwa amevujisha siri za uchawi, na kuhusu dawa alidai kuwa wameisha ziondosha zote. Mombi yaliendelea tena na kuamuliwa atoe kila kitu chocote ambacho amekabidhiwa……....



Visa hivi vinasikitisha nimejaribu kupunguza maelezo, ila ukisimuliwa inauma na inasikitisha sana binadamu si wema, angalizo ni kuwa tuwe makini na wasichana wa kazi kuwa wengine wanatumiwa bila kujijua.....

Tujajadili tusipuuzie maana wengi yanawakuta ila wanakaa kimya…..

No comments: