MJAMZITO, Mkazi wa kijiji cha kilimahewa kata ya nyangao katika Halmashauri ya Lindi vijijini Amina Sidi Seif (24), amekufa papo hapo kwa kupigwa na radi wakati akikinga maji ya mvua kubwa zilizokuwa aikinyesha kwenye nyumba jirani yake, Ofisa Mtedaji wa Kata ya Nyangao, Hawa Makwita amesema kuwa Amina ambaye alikuwa na mimba ya miezi mitano, alikufa kwa kupigwa na radi Machi 21 mwaka huu, majira ya saa 12:00 jioni. Makwita, alisema wakati akiwa katika harakati za kukinga maji hayo wakati mvua kubwa zikinyesha, radi kali ilimpiga mjamzito huyo na kufa papo hapo.
Kutoka Mkoa wa Lindi
Chanzo NIPASHE 23/3/2010
1 comment:
Jaman, kama kusingekuwa na kero ya maji huenda mama huyu asingekufa. Mungu amlaze pema peponi
Post a Comment