March 23, 2010

KIBOKO AJERUHI

JUMA Ally Mkuruge (32) Mkazi wa kata ya Samonga Wilaya ya Kilwa, amelezwa katika Hospitali ya Kinyonga kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa kwa kug'atwa paja la kulia na kiboko wakati akisafisha shamba lake.

Mama mzazi wa mejeruhi huyo, Binti Juma, alisema Mkureje alishambuliwa na Kiboko huyo ijumaa aliyopita majira ya saa 1.30 Asubuhi wakati akifyeka nyasi katika shamba hilo lilopo jirani na bwawa la maji.

Alisema, Kiboko huyo alitoka kwenye bwawa hilo na kumvamia mwanae kisha mumjeruhi kwa kumg'ata kwenye paja  "kwa kweli namshukuru Mungu kiboko yule amenyofoa nyama tu, hakuwahi kuvunja mfupa wa mguu wake, kwani kama angefanikiwa kuuvunja angekuwa mlemavu wa kudumu katika kipindi chote cha maisha yake" alisema.

No comments: