May 11, 2013

...MSHUKURU HUYU MTOTO!!! ...Vinginevyo nisingekuoa....!

Mshukuru huyu Mtoto, Vinginevyo nisingekuoa!!

Inasikitisha na inauma binti anavyoambiwa na Mumewe kuwa mshukuru huyu motto...vinginevyo nisingekuoa....! ka msemo huu, huwa Napata maswali mengi je wewe nani alikutuma umbebeshe mimba? nani alikushauri umtongoze kama ulikuwa humtaki? na nini kilikuwasha mpaka ukavutiwa naye... mpaka unamsimanga mtoto wa mwenzio kana kwamba wewe ulijiumba? je unafikiri kama wewe baba yako angemwambia mama yako ingekuwaje? je hiki sio chanzo cha kutafuta sababu za kumuacha mwenzio wakati tayari anamtoto wako? na kumsababishia msongo wa mawazo....?

Hebu wavulana acheni tabia hizi ambazo hazisaidii kabisa katika msitakhabari wa malezi ya watoto

Leo hii wazazi wanalalama kuwa watoto wetu wanaharibika hivi unamlaumu nani? wewe kama mzazi unawajibika vipi kuwalea watoto wa wenzio?au unawageuza wakubwa wenzio na wako unawalea vipi? maswali haya yananisumbua sana......




No comments: