Katika hali isiyo ya kawaida mkazi mmoja wa wilayani Kibha na mmiliki wa Gari aina ya Collora Sprinter amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutembea na nyoka katika gari yake kwa zaidi ya siku mbili. Nyoka huyo alimuona katika gari yake wakati alipokua anafungua buti la nyuma la gari yake. Mmiliki huyo ambaye hakupenda kujitambulisha jina lakealipatwa na mkasa huo alipokua amepaki gari lake maeneo ya Kibaha Picha ya ndege, alimuona nyoka mkubwa aina ya Swila alipokua anafungua buti ili kuchukua kidumu kwa ajili ya kununulia mafuta ya taa, baada ya kumuona nyoka huyo alipiga kelele huku akitetemeka na kupelekea wasamari wema kufika ili kutoa msaada, wakati wanajiandaa kumpiga nyoka huyo aliingia ndani ya gari kupitia kwenye tundu la Speaker.
Wasamaria walipedekeza kufungua milango ya gari, suala ambalo mmiliki huyo aliafiki ila baada ya kufungua milango na kumwaga mafuta ya taa kuzunguka eneo ilipopaki gari hiyo, nyoka huyo hakutoka wala kujitingisha. Alipoulizwa zaidi, mmiliki wa gari hilo alidai kua mara ya kwanza alimuona nyoka huyo ndani ya gari lake siku mbili zilizopita akiwa amepaki gari hilo nyumbani kwake, alipofanya jitihada za kutaka kumuua nyoka huyo alipotelea kwenye viti na kapeti zilizokuwemo ndani humo na baadae kutokuonekana kabisa.
Baadhi ya mashuhuda walieleza kuwa ni vigumu sana na haiwezekani nyoka kukaa katika gari ambayo ni nzima na inatembea kwa kuwa nyoka siku zote hapatani na harufu ya mafuta ya gari, hivyo kuwepo na kuishi kwa nyoka huyo katika gari ambalo linatembea kwa muda wa zaidi ya siku mbili kumezua maswali mengi miongoni mwa wanajamii wa maeneo ya kibaha picha ya ndege.... Na inasemekana kuwa nyoka huyo ni wa kimazingara suala ambalo mmiliki huyo hakutaka kukubaliana nalo..................Mpaka tunatoka eneo la tukio mida ya saa 12:20 Jioni gari hilo lilikuwa limepaki... na mmiliki wa gari....akiwa hajui la kufanya.
No comments:
Post a Comment